Indirimbo Zikundwa Open in the app

#129

Ninataka kumsifu Yesu Kristo

Wokovu

Couplet 1

Ninataka kumsifu Yesu Kristo aliyeondoa dhambi zangu zote. Twende sote sasa tumsifu Yeye, na Pendo kubwa la Mwokozi!

Refrain

Haleluya! Yu Mfalme ’kuu! Haleluya! Asifiwe! Alinisamehe dhambi zote; alinilinda kwa salama!

Couplet 2

Na baraka yake anaimimina, kama mvua inyeshavyo juu yangu. Nastarehe mikononi mwake Yesu, rehema yake inatosha.

Refrain

Haleluya! Yu Mfalme ’kuu! Haleluya! Asifiwe! Alinisamehe dhambi zote; alinilinda kwa salama!

Couplet 3

Siku moja nitamwona Yesu Kristo kati’ nchi nzuri sana ya furaha, macho yangu yatamtazama yeye, kuona sura ya Mfalme.

Refrain

Haleluya! Yu Mfalme ’kuu! Haleluya! Asifiwe! Alinisamehe dhambi zote; alinilinda kwa salama!