Indirimbo Zikundwa Open in the app

#128

Nina rafiki Mwema

Wokovu

Couplet 1

Nina rafiki Mwema, naye alinifilia; alinivuta kwake na amenifanya mpya. Ni mali yake Yesu tu, ninaongozwa naye, alikomboa mimi kwa agano la upendo.

Couplet 2

Nina rafiki Mwema, na aliondoa dhambi, aliniweka huru na kunipa Roho yake. Na vitu vyote ninavyo ninavitoa kwake, maisha yangu ni yake, yaimba sifa zake.

Couplet 3

Nina rafiki Mwema na anayeweza yote, pamoja naye Yesu tu nashinda majaribu, atanitwaa kwake ju’ Mbinguni kwa furaha; Nitastarehe katika makao ya milele.