Indirimbo Zikundwa Open in the app

#130

Ninataka kumsifu Yesu Bwana

Wokovu

Couplet 1

Ninataka kumsifu Yesu, Bwana wangu Mwema. Aliteswa hata kufa, ili niwe huru kweli.

Refrain

Mwimbieni Bwana Yesu kwa upendo wake ’kubwa! Alilipa deni langu, nimewekwa huru kweli.

Couplet 2

Ninataka ’shuhudia Pendo kubwa la Mwokozi, jinsi alivyoniponya nilipopotea mbali.

Refrain

Mwimbieni Bwana Yesu kwa upendo wake ’kubwa! Alilipa deni langu, nimewekwa huru kweli.

Couplet 3

Ninasifu Mwokozi kwa uwezo wake bora; naye anitia nguvu nimshinde yule mwovu.

Refrain

Mwimbieni Bwana Yesu kwa upendo wake ’kubwa! Alilipa deni langu, nimewekwa huru kweli.

Couplet 4

Ninataka kumwimbia Yesu Kristo, Bwana wangu. Aliniokoa kweli, niwe heri siku zote.