Indirimbo Zikundwa Open in the app

#118

Ni Mwokozi Mzuri ninaye

Wokovu

Couplet 1

Ni Mwokozi Mzuri ninaye, alikufa kunikomboa. Alitoa uzima wake kwa ajili ya watu wote.

Refrain

Alikufa Msalabani, alikufa Msalabani. Kwa ajili ya dhambi zangu zote alikufa Msalabani.

Couplet 2

Aliacha makao juu, akafika ulimwenguni; aliteswa kwa’jili yangu na kunifungulia Mbingu.

Refrain

Alikufa Msalabani, alikufa Msalabani. Kwa ajili ya dhambi zangu zote alikufa Msalabani.

Couplet 3

Dhambi zangu ali’chukua, kujitwika hukumu yangu, na alijeruhiwa ili aniponye na ’nipa raha.

Refrain

Alikufa Msalabani, alikufa Msalabani. Kwa ajili ya dhambi zangu zote alikufa Msalabani.

Couplet 4

Bwana Yesu alifufuka, akarudi Mbinguni kwake; na yuaja upesi tena achukue walio wake.