#119
Tuimbie Msalaba wa Mwokozi
Wokovu
Couplet 1
Tuimbie Msalaba wa Mwokozi, Damu yake inatusafisha sana! Tunaweza kuwa huru, kwani Yesu alikufa ili ku’ondoa dhambi.
Refrain
Haleluya, anipenda! Haleluya nafurahi! Haleluya, siku moja nitamwona Yesu!
Couplet 2
Twafurahi kwa Neema yake kubwa, alikuja ili tuwe na uzima. Kama njia ni nyembamba duniani, Yesu atatupa nguvu na ’hodari.
Refrain
Haleluya, anipenda! Haleluya nafurahi! Haleluya, siku moja nitamwona Yesu!
Couplet 3
Tuuimbe Moto ule ’takatifu uli’tupwa na Mwokozi duniani! Tuvipige vita vilivyo vizuri, nasi tutapewa taji ya uzima!
Refrain
Haleluya, anipenda! Haleluya nafurahi! Haleluya, siku moja nitamwona Yesu!