#117
Nilipofika Golgotha
Wokovu
Couplet 1
Nilipofika Golgotha nikaiona huko Neema kubwa kama mto, Neema ya ajabu.
Refrain
Neema ya Golgotha ni kama bahari kubwa, ne’ma tele na ya milele, ne’ma ya kutosha!
Couplet 2
Nilipofika moyo wangu ulilemewa sana, sikufaamu bado vema Neema yake kubwa.
Refrain
Neema ya Golgotha ni kama bahari kubwa, ne’ma tele na ya milele, ne’ma ya kutosha!
Couplet 3
Nilipoona kwamba Yesu alichukua dhambi, Neema ikadhihirika, na moyo ukapona.
Refrain
Neema ya Golgotha ni kama bahari kubwa, ne’ma tele na ya milele, ne’ma ya kutosha!
Couplet 4
Mbinguni nitakapofika, furaha itakuwa kuimba juu ya Neema milele na milele.