#116
Tuimbie, tumsifu Yesu
Wokovu
Couplet 1
Tuimbie, tumsifu Yesu ju’ya Msalaba! Aliteswa na akafa, yote kwa ajili yetu. Akashinda, ’kafufuka, ni Mwokozi ’kamilifu.
Refrain
Yesu alitukomboa, na akawa haki yetu. Dhambi aliziondoa, akatupa tumaini: Tutarithi utukufu, nuru, raha na uheri.
Couplet 2
Yesu alipofufuka akatushindia kufa, akapewa nguvu zote duniani na Mbinguni. Sisi sote tumepona kwa kupigwa kwake Yesu.
Refrain
Yesu alitukomboa, na akawa haki yetu. Dhambi aliziondoa, akatupa tumaini: Tutarithi utukufu, nuru, raha na uheri.
Couplet 3
Tushukuru Mungu Baba kwa ajili ya upendo! Tumsifu Yesu Kristo kwa Neema yake kubwa! Tumfungulie moyo kwake Roho ’takatifu!
Refrain
Yesu alitukomboa, na akawa haki yetu. Dhambi aliziondoa, akatupa tumaini: Tutarithi utukufu, nuru, raha na uheri.