#107
Alipoteswa Yesu peke’
Wokovu
Couplet 1
Alipoteswa Yesu peke’ katika Gethsemane, akakinywea kwa upendo kikombe cha uchungu.
Refrain
Mwokozi wangu alichukua yote, uzima wake ali’toa; kutuokoa alitufilia.
Couplet 2
Akasimama peke yake kuchekwa na kupigwa, uchwani akatiwa taji iliyo ya miiba.
Refrain
Mwokozi wangu alichukua yote, uzima wake ali’toa; kutuokoa alitufilia.
Couplet 3
Akachukua Msalaba njiani kwa Golgotha, na akajeruhiwa sana kwa’jili yetu sisi.
Refrain
Mwokozi wangu alichukua yote, uzima wake ali’toa; kutuokoa alitufilia.
Couplet 4
Na sasa, wewe mwenye dhambi, tazama pendo lake! Neema kubwa yakungoja; uache dhambi zako!
Refrain
Mwokozi wangu alichukua yote, uzima wake ali’toa; kutuokoa alitufilia.