Indirimbo Zikundwa Open in the app

#106

Tuimbe asubuhi hii

Wokovu

Couplet 1

Tuimbe asubuhi hii juu ya siku manabii walioitabiri! Ni siku kubwa, siku nzuri, upendo umedhihirika, upendo wake Mungu. Sisi sote tufurahi, tumwimbie na kusifu Yesu, Mwokozi wetu!

Couplet 2

Yu sura yake Mungu Baba, lakini mtu, ili sisi tupate kumjua. Yuaja na amani kwetu, Kuwatafuta wapotevu na kuwaponya wote. Sisi sote tuungane naye Yesu na tupate pendo na uzima wake!

Couplet 3

Ataliona sikitiko, na kufahamu shida yetu asaidie sisi! Atafundisha haki kweli, kweli, Nakutufahamisha pendo katika kufa kwake, sisi sote tuokoke, na tufufuliwe naye, Mbingu zitufunguliwe!