#96
Mwokozi wetu aliahidi
Wokovu
Couplet 1
Mwokozi wetu aliahidi ya kwamba atakuja siku moja kutupeleka Mbinguni kwake. Yawezekana upesi sana.
Refrain
Sioni shida, nina amani kwa Mkombozi na Damu yake, na Roho yake Mtakatifu ni arabuni ya ’rithi yangu.
Couplet 2
Wajumbe wengi wa Bwana Mungu watumwa sasa duniani pote. Waitangaza habari njema ya Yesu Kristo na pendo lake.
Refrain
Sioni shida, nina amani kwa Mkombozi na Damu yake, na Roho yake Mtakatifu ni arabuni ya ’rithi yangu.
Couplet 3
Na watu wengi wanaamini, wanaitika mwito wake Mungu. Kwa roho moja twa kaza mwendo, tufikilie thawabu yetu.
Refrain
Sioni shida, nina amani kwa Mkombozi na Damu yake, na Roho yake Mtakatifu ni arabuni ya ’rithi yangu.
Couplet 4
Twakaribia wakati ule wa kuja kwake Bwanda Yesu Kristo; na tujiweke tayari wote kuchukuliwa Mbinguni kwake!