Indirimbo Zikundwa Open in the app

#95

Nchi nzuri yatungoja huku juu

Wokovu

Couplet 1

Nchi nzuri yatungoja huko juu ya mawingu, watakapokusanyika wateule. Siku zina’tubakia zinapita mbio sana; waminifu watarithi nchi nzuri.

Refrain

:/: Lo! Ufalme wake Mungu u karibu!:/: Uwe safi, roho yangu, ukakeshe siku zote! Lo! Mfalme wake Yesu yu karibu!

Couplet 2

Twaamini tutaona nchi ile kwa uwazi, tunangoja sana Mkombozi wetu; kwa dalili tunaona siku yake ni karibu; zinatuarifu Yesu aja hima.

Refrain

:/: Lo! Ufalme wake Mungu u karibu!:/: Uwe safi, roho yangu, ukakeshe siku zote! Lo! Mfalme wake Yesu yu karibu!

Couplet 3

Maandiko yanasema: Mkombozi atakuja, katika mawingu ataonekana. Haleluya! Haleluya! Atafunga yule mwovu, aliyejaribu kutuangamiza.

Refrain

:/: Lo! Ufalme wake Mungu u karibu!:/: Uwe safi, roho yangu, ukakeshe siku zote! Lo! Mfalme wake Yesu yu karibu!

Couplet 4

Katika kungoja Yesu watu wengi wamechoka; waamshe, uwaonye kwa dalili! Kwani neno lake Mungu latimizwa mbio sana, tunaona kwamba Yesu yu karibu.

Refrain

:/: Lo! Ufalme wake Mungu u karibu!:/: Uwe safi, roho yangu, ukakeshe siku zote! Lo! Mfalme wake Yesu yu karibu!