#97
Bado kidogo jua litapanda
Wokovu
Couplet 1
Bado kidogo jua litapanda, siku tuta’pofika huko juu. Huko Mbinguni tutapumzika na’pata raha na furaha ya milele.
Refrain
Tutamlaki Bwana Yesu Kristo, aliyetuokoa kweli hapa chini. Huko Mbinguni tutamwona yeye, tutamsifu kwa upendo wake ’kuu.
Couplet 2
Bado kidogo tutaona vyote vitageuka kuwa vipya tena, na hapo, Yesu, Mwokozi wetu, atatufungulia lango la Mbinguni.
Refrain
Tutamlaki Bwana Yesu Kristo, aliyetuokoa kweli hapa chini. Huko Mbinguni tutamwona yeye, tutamsifu kwa upendo wake ’kuu.
Couplet 3
Safari yetu ina majaribu, tutafurahi kwa kufika Mbingu. Hatutaona giza, shaka tena, Tutamshangilia Mwokozi wetu.