Indirimbo Zikundwa Open in the app

#84

Ninakumbuka Sayuni

Wokovu

Couplet 1

Ninakumbuka Sayuni, nchi ya heri Mbinguni, bahari kama kioo na’furahia rohoni. Nyuma kimeta cha nuru Naona mji wa Mbingu, nyimbo za nyumba ya Baba nasikiliza daima.

Refrain

Mapambazuko Mbinguni yataondoa utaji, vyote tulivyoamini tutaviona milele.

Couplet 2

Mauti haina nguvu, Yesu a’vunja uchungu, naye aliwakomboa wote; wafalme, watumwa. Ninamtwika Mwokozi dhambi, huzuni na shida; mbavuni mwake nafasi kama bandari salama.

Refrain

Mapambazuko Mbinguni yataondoa utaji, vyote tulivyoamini tutaviona milele.

Couplet 3

Kuna ’jaribu njiani, mengi yakunizuia, na mara nyingi miiba, inaumiza miguu. Nikikumbuka Sayuni moyo huwaka kabisa, Mbingu ninaitazama na ku’himiza safari.

Refrain

Mapambazuko Mbinguni yataondoa utaji, vyote tulivyoamini tutaviona milele.