#85
Twapasha habari ya Mbingu
Wokovu
Couplet 1
Twapasha habari ya Mbingu, mahali pa watu wa heri, na tunatamani ku’ona ufuko wa nchi ya Mbingu.
Refrain
Sikitiko, wala shida hazitakuwapo Mbinguni. Huko juu, huko juu tutashangilia milele.
Couplet 2
Twapasha habari ya Mbingu na mji mzuri ajabu, na jeshi la watakatifu waliomaliza safari.
Refrain
Sikitiko, wala shida hazitakuwapo Mbinguni. Huko juu, huko juu tutashangilia milele.
Couplet 3
Twapasha habari ya pendo, amani na nguo nyeupe. na raha baada ya vita, makao karibu na Mungu.
Refrain
Sikitiko, wala shida hazitakuwapo Mbinguni. Huko juu, huko juu tutashangilia milele.
Couplet 4
Twapasha habari ya Yesu, alituokoa na dhambi. Ingawa ni shida njiani atatufikisha Mbinguni.