#83
Ninajua nchi huko juu
Wokovu
Couplet 1
Ninajua nchi huko juu, hapo Mungu alijenga mji, na aita ’moma moja kwake, waliomaliza mwendo huku.
Refrain
Shida, kufa na huzuni hazitakuwapo huko. Yesu atafuta kila chozi, tutaona shangwe, nayo tele.
Couplet 2
Huko hawataingia kamwe wenye dhambi, wala cha kinyonge, E’ rafiki, ujihoji leo kama wewe utaona Mbingu!
Refrain
Shida, kufa na huzuni hazitakuwapo huko. Yesu atafuta kila chozi, tutaona shangwe, nayo tele.
Couplet 3
Utazame, mto ungaliko uwezao kusafisha sana! Ujioshe kati’ Damu safi ya Mwokozi wetu Yesu Kristo!
Refrain
Shida, kufa na huzuni hazitakuwapo huko. Yesu atafuta kila chozi, tutaona shangwe, nayo tele.
Couplet 4
Nafurahi kwani ninajua kao langu liko huko juu, natamani sana kufikako. Njoo, Yesu, unitwae mbio.