Indirimbo Zikundwa Open in the app

#78

Nina uzima wa milele

Wokovu

Couplet 1

Nina uzima wa milele, na tumaini ni imara, Mbinguni nitaona Yesu, Mwokozi wangu kwa furaha.

Couplet 2

Nina urithi bora huko unaolindwa hata mwisho. Na kila siku ya jaribu natiwa nguvu naye Baba.

Couplet 3

Namshukuru Mungu wangu! Ananitunza siku zote katika shida na taabu, kwa hiyo sisumbuki tena.

Couplet 4

Rohoni mwangu ni amani, naimba kwa furaha kubwa. Nikiongozwa naye Yesu naendelea kwa salama.

Couplet 5

E’ Bwana Yesu, unifunze ku’tumikia wewe vema wakati ubakio tena wa mwendo wangu dunianai!