Indirimbo Zikundwa Open in the app

#77

Naifuata njia ya ku’fikia Mbingu

Wokovu

Couplet 1

Naifuata njia ya kufikia Mbingu na mji Mwema ule alio’jenga Mungu. Ninasafiri sasa kutoka duniani nifikie nchi hiyo ya raha na uzima.

Refrain

Naifuata njia ya ku’fikia Mbingu na mji Mwema ule alio’jenga Mungu.

Couplet 2

Sijauona bado uzuri wake bora wa mji wa Mbinguni, usio na machozi; lakini siku moja, kwa shangwe ya milele nitamsifu Yesu katika mji ule.

Refrain

Naifuata njia ya ku’fikia Mbingu na mji Mwema ule alio’jenga Mungu.

Couplet 3

Nifikapo mjini, mlango wake wazi, na hapo malaika watanikaribisha; shindano la dunia halitakuwa huko, na nitaona raha milele na milele.

Refrain

Naifuata njia ya ku’fikia Mbingu na mji Mwema ule alio’jenga Mungu.