Indirimbo Zikundwa Open in the app

#79

Maisha ya mtu [mafupi] ya hapa

Wokovu

Couplet 1

Maisha ya mtu [mafupi] ya hapa dunia yanaifanana safari chomboni. Twapita bahari katika hatari, lakini Mwokozi anatuongoza.

Refrain

Ikiwa Mwokozi anatuongoza twaweza kuona amani na raha, atatufikisha salama Mbinguni, na humo hatutakumbuka safari.

Couplet 2

Twapita katika baridi na pepo, maneno ya Mungu ni nuri gizani. Hatari na hofu na chombo kibaya hatuta’kumbuka karibu na Yesu.

Refrain

Ikiwa Mwokozi anatuongoza twaweza kuona amani na raha, atatufikisha salama Mbinguni, na humo hatutakumbuka safari.

Couplet 3

Ingawa mawimbi yapiga kwa nguvu, tunakaribia bandari upesi. Na humo hakuna dhoruba na pepo; safari tutaimaliza salama.

Refrain

Ikiwa Mwokozi anatuongoza twaweza kuona amani na raha, atatufikisha salama Mbinguni, na humo hatutakumbuka safari.

Couplet 4

Tutakapofika bandari ya Mbingu tutamshukuru Mwokozi mkuu. Hatutaziona hatari na hofu karibu na Yesu mwenyewe Mbinguni.