#76
Mgeni mimi, ninasafiri
Wokovu
Couplet 1
Mgeni mimi, ninasafiri siku chache, siku chache huku chini. Msinipinge, niwafuate watakatifu walioshinda! Mgeni mimi, ninasafiri siku chache, siku chache huku chini.
Couplet 2
Nashika njia, napiga mbio, sina budi kuukuza mwendo wangu. Na kwa mkono natwaa gongo, nazo silaha nimejivika. Nashika njia, napiga mbio, sina budi kuukuza mwendo wangu.
Couplet 3
Ulimwenguni sipati raha, natamani ku’fikia mji mpya. Machozi, kufa, maombolezo sitayaona Mbinguni tena. Ulimwenguni sipati raha, natamani ku’fikia mji mpya.
Couplet 4
Mchunga Mwema, ninakuomba, ’tangulie, niongoze njia yote, kwa kuwa giza na dhambi tena zaniwekea mitego mingi! Mchunga Mwema, ninakuomba, ’tangulie, niongoze njia yote!