#75
Niliye msafiri, mgeni duniani
Wokovu
Couplet 1
Niliye msafiri, mgeni duniani; sioni kwangu hapa, ni huko ju’ Mbinguni. Ninatamani nami kukaa siku zote pamoja naye Baba katika utukufu.
Refrain
{Kwangu Mbinguni, kwangu,} x2 Uzuri wa Mbinguni wapita yote huku.
Couplet 2
Mwokozi yuko huko, rafiki yangu Mwema, aliyenikomboa na ku’chukua dhambi. Na hata nikiona furaha siku zote ningali natamani makao ya Mbinguni.
Refrain
{Kwangu Mbinguni, kwangu,} x2 Uzuri wa Mbinguni wapita yote huku.
Couplet 3
Na nikipewa huku vipawa vya thamani, na wakiimba nyimbo za kunifurahisha, rafiki wangu wote wakipendeza mimi, ningali natamani makao ya Mbinguni.
Refrain
{Kwangu Mbinguni, kwangu,} x2 Uzuri wa Mbinguni wapita yote huku.
Couplet 4
Upesi nitaona kifiko cha Mbinguni, Mwokozi wangu Yesu atanikaribisha; Na huko nitaona nilivyotumaini, kinubi nita’piga kumshukuru Yesu.
Refrain
{Kwangu Mbinguni, kwangu,} x2 Uzuri wa Mbinguni wapita yote huku.