#69
Je, tutaonana tena huko ng’ambo
Wokovu
Couplet 1
Je, tutaonana tena huko ng’ambo ya Yordani, na pamoja na Wakristo ’ona raha ya milele?
Refrain
Tuonane, tuonane huko ng’ambo ya bahari! Tuonane kwa furaha, huko shida ikomapo!
Couplet 2
Je, tutaonana tena, ba’da ya dhoruba zote huko katika bandari ya salama na amani?
Refrain
Tuonane, tuonane huko ng’ambo ya bahari! Tuonane kwa furaha, huko shida ikomapo!
Couplet 3
Je, tutaonana tena kati’ mji wa dhahabu, Penye mto wa uzima nayo miti ya matunda?
Refrain
Tuonane, tuonane huko ng’ambo ya bahari! Tuonane kwa furaha, huko shida ikomapo!
Couplet 4
Je, tutaonana tena na kusifu Mungu wetu miongoni mwa Wakristo waimbao huko juu?
Refrain
Tuonane, tuonane huko ng’ambo ya bahari! Tuonane kwa furaha, huko shida ikomapo!
Couplet 5
Tutaona na wapenzi waliotuacha huku? Je, tutawaona wote katika makao mema?
Refrain
Tuonane, tuonane huko ng’ambo ya bahari! Tuonane kwa furaha, huko shida ikomapo!
Couplet 6
Tutaona Bwana Yesu katika kutano huko, tutakaribishwa naye katika karamu kuu.