Indirimbo Zikundwa Open in the app

#68

Mbinguni kwa Mwokozi wangu

Wokovu

Couplet 1

Mbinguni kwa Mwokozi wangu Mwema nitaamka asubuhi moja, Nitayaona majeraha yake, sauti yake nitaisikia.

Couplet 2

Makao ya milele ni tayari, ali’waandalia watu wake. Tutamsifu Yesu sana huko, aliyetuokoa na hatari.

Couplet 3

Na nyimbo za Wokovu zinaimbwa Mbinguni mbele ya Mwokozi wetu; tungesikia huku nusu ndogo, vitani tungepata ushujaa.

Couplet 4

Lakini Yesu yupo nasi leo, usiku kama Moto mbele yetu. Na neno lake, ni upanga wetu, ahadi ni safina ju’ ya maji.

Couplet 5

Tungoje Yesu siku chache tena! Twakaribia mwisho wa safari. Tungoje asubuhi huko juu! Atatukaribisha Bwana Yesu!