#70
Kuna mji huko juu
Wokovu
Couplet 1
Kuna mji huko juu, umejengwa naye Mungu, humo kuna mto ’moja wenye maji mazima kabisa.
Refrain
Tutakusanyika huko kwa raha penye mto Mwema sana, tutakusanyika na Wakristo penye mto wa maji mazima.
Couplet 2
Huko pwani nchi nzuri, bila dhambi na huzuni, tutaimba nyimbo mpya, nyimbo njema ’kusifu Mwokozi.
Refrain
Tutakusanyika huko kwa raha penye mto Mwema sana, tutakusanyika na Wakristo penye mto wa maji mazima.
Couplet 3
Kama twamwamini Yesu, kama hatufichi dhambi, kama moyo ni mweupe, tutafika mtoni pa Mbingu.
Refrain
Tutakusanyika huko kwa raha penye mto Mwema sana, tutakusanyika na Wakristo penye mto wa maji mazima.
Couplet 4
Tu karibu ya kufika na kuona mto ule, Mungu atatupa raha na kutustarehesha daima.