#60
Ni heri kuona ndugu
Wokovu
Couplet 1
Ni heri kuona ndugu njiani pa kwenda Mbingu. Tukinyong’onyea sana kwa kuwa tu peke yetu, kushirikiana kwa ndugu kunaturudisha moyo, na Mungu atupa nguvu tukiyainua macho.
Couplet 2
Twafungamana rohoni, tulio wa nyumba yake, huoni ulimwenguni kushirikiana kwetu. Na tuna Mwokokozi mmoja, imani ni moja pia, watoto wa Baba ’moja twashika sheria yake.
Couplet 3
Furaha ya ulimwengu haitatuvuta tena, Twaona kung’aa kwake ni bure na bila kisa. Lakini tukikusanyika kwa jina la Mungu Baba, atuandalia kweli karamu ilio bora.
Couplet 4
Tukivumilia hata ukomo wa mashindano, Mbinguni tutawaona Wakristo wapenzi wote. Hatutatawanyika huko, tu wote umoja kweli, milele tuta’pokaa nyumbani kwa Baba yetu.