#59
Yesu, ninakutolea, moyo na maisha
Wokovu
Couplet 1
Yesu, ninakutolea, moyo na maisha yangu, niwe mfuasi wako, Safi na mtakatifu.
Refrain
:/: Mungu wangu, Mungu wangu, nitakase saa hii! :/:
Couplet 2
E’ Mwokozi, nitakase, unijaze Pendo lako. Na maisha yangu yote yawe yako, Bwana wangu!
Refrain
:/: Mungu wangu, Mungu wangu, nitakase saa hii! :/:
Couplet 3
Ninataka kuheshimu wewe, Mkobozi Mwema; nifanane nawe, Yesu, kati’ watu wa dunia!
Refrain
:/: Mungu wangu, Mungu wangu, nitakase saa hii! :/:
Couplet 4
Nikikaa kimya kwako kama yule Mariamu, nifundishwe nawe, Bwana, sitahangaika tena.
Refrain
:/: Mungu wangu, Mungu wangu, nitakase saa hii! :/:
Couplet 5
Tawi lake mzabibu, ulitunze na ’safisha, ili kwa uwezo wako litaza’ matunda mengi!
Refrain
:/: Mungu wangu, Mungu wangu, nitakase saa hii! :/: