Indirimbo Zikundwa Open in the app

#61

Enyi watu wa Sayuni

Wokovu

Couplet 1

Enyi watu wa Sayuni, kundi dogo la Mwokozi, Yesu aliwanunua kuwa mali yake Mungu. Sasa mnapita njia ya miiba na hatari kati’ nchi ya ugeni; bali Mbingu mtafika.

Couplet 2

Kumwamini, kumpenda Yesu ni uheri wetu; amri zote zinashikwa kwa upendo na amani. Kwa imani twaokoka, pendo ni uzima wetu. Yesu utusaidie, utujaze Pendo lako!

Couplet 3

Juu ya msingi huo, Yesu, unijenge mimi, na zaidi niungane nawe na kanisa lako! Sisi tu matawi yako, tushirikiane sana, na katika kundi nzima iwe nia moja kweli!