#52
Kwa salama Baba Mungu
Wokovu
Couplet 1
Kwa salama Baba Mungu awalinda watu wake, hata nyota za Mbinguni si salama kama wao.
Couplet 2
Mungu awalinda hivyo katika upendo wake. Wanakumbatiwa naye, wanarehemiwa sana.
Couplet 3
Hawavutwi toka kwake kwa furaha wala shida. Yeye ni rafiki ’kubwa wa walio watu wake.
Couplet 4
Wanalishwa, wanavikwa, wanafarijiwa naye. Hata nywele za kichwani zimehesabiwa zote.
Couplet 5
Enyi kundi lake dogo, Mungu atawahifadhi! Na adui watashindwa kwa uwezo wake ’kubwa.
Couplet 6
Akitoa, akiwapa, Baba yetu hageuki. Na mapenzi yake ndiyo: Wana wapatishwe wema.