Indirimbo Zikundwa Open in the app

#51

Naona amani Golgotha

Wokovu

Couplet 1

Naona amani Golgotha alipojitoa Mwokozi, :/:Na huko nina kimbilio kwa Yesu aliyejitoa.:/:

Couplet 2

Sitaki ’tamani fahari na dhambi katika dunia, :/: Sababu Wokovu ninao katika ’jeraha ya Yesu. :/:

Couplet 3

Aliziondoa kabisa mizigo na kamba ya dhambi. :/: Na niliokoka halisi kwa neno la Mungu wa ’hai. :/:

Couplet 4

Maneno ya Mungu ni kwetu chakula na dawa ya roho, :/: na nguvu ya kusaidia Mkristo katika safari. :/:

Couplet 5

Mimi sasa hekalu la Roho, anayemiliki moyoni; :/: na Yesu ataniongoza kwa njia ya ahadi zake. :/:

Couplet 6

Uliye dhambini ufike kwa Yesu Mwokozi wa wote! :/: Anakunyoshea mikono ya pendo kukusaidia. :/: