#53
Kati’ mikono yake Yesu
Wokovu
Couplet 1
Kati’ mikono yake Yesu ananilinda. Katika Pendo kubwa ninapumzika sana. Sasa sauti nzuri itokeayo juu inanikumbukia Mbingu na raha yake.
Refrain
Kati’ mikono yake Yesu ananilinda. Katika Pendo kubwa ninapumzika sana.
Couplet 2
Kati’ mikono yake nitakaa daima, sitatetema tena, yeye ni uwezo wangu. Shaka sinayo sasa, wala sioni woga, hata ikiwa shida, Yesu anifariji.
Refrain
Kati’ mikono yake Yesu ananilinda. Katika Pendo kubwa ninapumzika sana.
Couplet 3
Yesu Mwokozi wangu alikombo mimi, Ufa wa Mwamba ule, nitapumzika humo. Katika saa ngumu ya majaribu tele ninasaburi’ona jua la asubuhi.
Refrain
Kati’ mikono yake Yesu ananilinda. Katika Pendo kubwa ninapumzika sana.