Indirimbo Zikundwa Open in the app

#50

Sitasumbuka kwa kuwa Mungu

Wokovu

Couplet 1

Sitasumbuka kwa kuwa Mungu ananitunza daima, anachukuwa mizigo yangu nyakati zote za mwendo.

Refrain

Sijaiona nyingine siku, na jana imetoweka, na leo Mungu anazijuwa hitaji zote ninazo.

Couplet 2

Sitasumbuka kwa kuwa Mungu ni Baba yangu kabisa. Hawezi kunisahau mimi ingawa akijificha.

Refrain

Sijaiona nyingine siku, na jana imetoweka, na leo Mungu anazijuwa hitaji zote ninazo.

Couplet 3

Sitasumbuka kwa kuwa Mungu anishibisha neema, anipa yote yanifaayo kwa roho yangu na mwili.

Refrain

Sijaiona nyingine siku, na jana imetoweka, na leo Mungu anazijuwa hitaji zote ninazo.

Couplet 4

Mauwa yote anayavika, Na ndege wote wa anga wanapokea chakula chao pasipo shamba na ghala.

Refrain

Sijaiona nyingine siku, na jana imetoweka, na leo Mungu anazijuwa hitaji zote ninazo.

Couplet 5

Ninafurahi katika Bwana, Na kama ndege naimba. Najuwa kwamba nyakati zote Babangu ananitunza.