Indirimbo Zikundwa Open in the app

#49

Njia yote naongozwa kwa mkono

Wokovu

Couplet 1

Njia yote naongozwa kwa mkono wa Mwokozi, ninapo wema wake, sina shaka, hofu tena. Nina raha ya Mbinguni, ninakaa kwa salama. :/: Na katika mambo yote ananitendea mema. :/:

Couplet 2

Njia yote naongozwa, namtegemea Yesu. Anilinda jaribuni, anitia nguvu pia. Nikiona kiu hapa, nikichoka safarini,:/: Mwamba uliopoasuka unabubujika maji. :/:

Couplet 3

Njia yote naongozwa kwa mkono wake bora, atanituliza tena kwa babake huko juu. Miguuni pake Yesu ninataka kusujudu,:/: Nakusifu yeye, kwani aliniongoza huku. :/: