Indirimbo Zikundwa Open in the app

#48

Siwezi mimi kufaamu sana

Wokovu

Couplet 1

Siwezi mimi kufaamu sana Neema yake Mungu kwangu, zamani nilikuwa mkosaji, lakini alinisamehe.

Refrain

Bali namjua Mungu, anayeweza kunilindia urithi wangu juu hata siku yake Yesu.

Couplet 2

Siwezi mimi kufaamu sana upendo wake ’kubwa mno; nimeamini neno lake kubwa kweli, na ninaona raha tele.

Refrain

Bali namjua Mungu, anayeweza kunilindia urithi wangu juu hata siku yake Yesu.

Couplet 3

Siwezi kufaamu kazi kubwa ya Roho yake ndani yetu, anayeweza kufundisha mtu kutegemea Yesu.

Refrain

Bali namjua Mungu, anayeweza kunilindia urithi wangu juu hata siku yake Yesu.

Couplet 4

Sijui mimi siku zangu tena za kutembea duniani. Na labda nitaona shida huku, taabu na huzuni nyingi.

Refrain

Bali namjua Mungu, anayeweza kunilindia urithi wangu juu hata siku yake Yesu.

Couplet 5

Sijui mimi kama siku moja nitakuona kufa huku, au kwa hima nitabadilika, ajapo Bwana na mawingu.

Refrain

Bali namjua Mungu, anayeweza kunilindia urithi wangu juu hata siku yake Yesu.