Indirimbo Zikundwa Open in the app

#44

Tu watu huru kweli

Wokovu

Couplet 1

Tu watu huru, huru kweli katika Yesu Kristo. Tunahubiri neno lake kwa Moto ’takatifu. Tuendelee, mbele, mbele, tukashinde majaribu! Twapiga vita ya imani, tuvumilie yote!

Couplet 2

Tu jeshi kubwa la askari, tu safi kati’ Damu. Mfalme wetu, Yesu Kristo, ni kiongozi wetu. Kwa nguvu yake kubwa mno tutadumu hata kufa. Tuendelee, mbele, mbele, tumshukuru Mungu.

Couplet 3

Kwa Yesu tuna uhodari na mamlaka kubwa, maana tunayaamini maneno yake yote. Kisima wazi, cha ajabu, kinatoka Msalaba, tuliyakunywa maji yake, ni maji ya uzima.

Couplet 4

Mbinguni nchi ya asili [raha], ya haki na amani, tuta’pofika huko juu tutamwimbia Yesu. Na kila chozi litafutwa na mkono wa Mwokozi. Kwa shangwe kubwa tutarithi ufalme wa ahadi.