Indirimbo Zikundwa Open in the app

#45

Waisraeli walika’ Babeli utumwani

Wokovu· Werner Skibstedt

Couplet 1

Waisraeli walika’ Babeli utumwani, wakawa na huzuni tu kwa ’jili ya Sayuni.

Refrain

Hapo amri ilifika waliweza kuondoka, shangwe gani mioyoni mwao! Walitwaa vinubi vyao, wakaenda wanaimba hadi, hata kurithi nchi yao.

Couplet 2

Vinubi havikubigwa wakati wa utumwa, na walikaa kimya tu mahali pa ugeni.

Refrain

Hapo amri ilifika waliweza kuondoka, shangwe gani mioyoni mwao! Walitwaa vinubi vyao, wakaenda wanaimba hadi, hata kurithi nchi yao.

Couplet 3

Walipotoka Babeli, ikawa kama ndoto; furaha nyingi rohoni, faraja na uheri.

Refrain

Hapo amri ilifika waliweza kuondoka, shangwe gani mioyoni mwao! Walitwaa vinubi vyao, wakaenda wanaimba hadi, hata kurithi nchi yao.

Couplet 4

Mataifa walisema: «Mungu umefanyaje? Watumwa wameondoka, wamewekwa huru»!

Refrain

Hapo amri ilifika waliweza kuondoka, shangwe gani mioyoni mwao! Walitwaa vinubi vyao, wakaenda wanaimba hadi, hata kurithi nchi yao.

Couplet 5

Katika ulimwengu hu’ ni wengi wafungwao. Uhuru ni kwa Yesu tu kwa kila a’miniye.

Refrain

Ngiye ameleta amri: Tunaweza kuondoka, shangwe ku’kwa kila ’aminiye! Njoo sasa, twa’ kinubi, tufuate kwa kuimba hata kuirithi nchi yetu!