Indirimbo Zikundwa Open in the app

#43

Juu ya Mwamba umejenga kanisa

Wokovu

Couplet 1

Juu ya Mwamba umejenga kanisa lako duniani, umeliweka huru kweli katika Damu yako, Yesu.

Refrain

Juu ya Mwamba, juu ya Mwamba huru na safi umelijenga. Juu ya Mwamba, juu ya Mwamba, huru na safi tusimame!

Couplet 2

Neema kubwa! Nimepata sehemu yangu kanisani. Vita ya roho imekwisha, umenijaza utulivu.

Refrain

Juu ya Mwamba, juu ya Mwamba huru na safi umelijenga. Juu ya Mwamba, juu ya Mwamba, huru na safi tusimame!

Couplet 3

Kati’ hekalu lake Mungu nimefanyika jiwe hai. Ninashiriki mwili wake kama kiungo chake Kristo.

Refrain

Juu ya Mwamba, juu ya Mwamba huru na safi umelijenga. Juu ya Mwamba, juu ya Mwamba, huru na safi tusimame!

Couplet 4

Ju’ ya msingi huo safi liwe kanisa lako zima! Vyote vikiondoka huku, litasimama, litashinda.