Indirimbo Zikundwa Open in the app

#42

Bwana Yesu amevunja minyororo

Wokovu

Couplet 1

Bwana Yesu amevunja minyororo ya maovu, nimewekwa huru kweli mbali na makosa yangu.

Refrain

Haleluya, haleluya! Yesu Kristo ni Mwokozi! Haleluya, haleluya! Yesu alinikomboa.

Couplet 2

Nilipoungama dhambi, nikawekwa huru kweli. Moyo wangu unawaka kwa upendo ’takatifu.

Refrain

Haleluya, haleluya! Yesu Kristo ni Mwokozi! Haleluya, haleluya! Yesu alinikomboa.

Couplet 3

Kamba zilizonifunga zimetoka, nafurahi. Dhambi zilizo ’sumbua zimetupwa mbali sana.

Refrain

Haleluya, haleluya! Yesu Kristo ni Mwokozi! Haleluya, haleluya! Yesu alinikomboa.

Couplet 4

Ninataka kuhubiri: Nimewekwa huru kweli. Nipeleke kwa furaha neno zuri la Mwokozi.

Refrain

Haleluya, haleluya! Yesu Kristo ni Mwokozi! Haleluya, haleluya! Yesu alinikomboa.