Indirimbo Zikundwa Open in the app

#40

Ameniweka huru kweli

Wokovu

Couplet 1

Ameniweka huru kweli, naimba sasa: Haleluya! Kwa Msalaba nimepata kutoka katika utumwa.

Refrain

Nimeokoka, nafurahi! Na dhambi zangu zimetoka. Nataka kumtumikia Mwokozi wangu siku zote.

Couplet 2

Zamani nilifungwa sana kwa minyororo ya shetani, nikamwendea Bwana Yesu, akaniweka huru kweli.

Refrain

Nimeokoka, nafurahi! Na dhambi zangu zimetoka. Nataka kumtumikia Mwokozi wangu siku zote.

Couplet 3

Neema kubwa nilipata kuacha njia ya mauti, na nguvu ya Wokovu huo yanichukua siku zote.

Refrain

Nimeokoka, nafurahi! Na dhambi zangu zimetoka. Nataka kumtumikia Mwokozi wangu siku zote.

Couplet 4

Na siku moja nitafika Mbinguni kwake Mungu wangu. Milele nitamhimidi na kumwimbia kwa shukrani.