Indirimbo Zikundwa Open in the app

#39

Yesu ameingia katika roho yangu

Wokovu

Couplet 1

Yesu ameingia katika roho yangu, amenifungulia kamba za dhambi zangu. Tena amenijaza Roho Mtakatifu. Ninamsifu sasa kwa wimbo mpya.

Refrain

Yesu ni yote kwangu, yote na’pata kwake. Ameondoa dhambi, ametakasa mimi. Shangwe rohoni mwangu ni kama maji mengi, namshukuru sana Mwokozi wangu.

Couplet 2

Siku si ndefu tena, kazi si ngumu sasa, njia yanipendeza, ’kiwa nyembamba sana. Katika hali zote ninamwimbia Yesu, yeye Mfalme wangu, ninamsifu!

Refrain

Yesu ni yote kwangu, yote na’pata kwake. Ameondoa dhambi, ametakasa mimi. Shangwe rohoni mwangu ni kama maji mengi, namshukuru sana Mwokozi wangu.

Couplet 3

Katika mwendo wangu ninazidishwa shangwe, hata wakinicheka, mwovu akijaribu. Hima Mwokozi wangu atanyakua mimi toka machoni pao. Haleluya!

Refrain

Yesu ni yote kwangu, yote na’pata kwake. Ameondoa dhambi, ametakasa mimi. Shangwe rohoni mwangu ni kama maji mengi, namshukuru sana Mwokozi wangu.