#35
Nimefika kwake Yesu
Wokovu
Couplet 1
Nimefika kwake Yesu, Na rohoni mwangu sasa, jua lake la Neema linang’aa kila siku.
Refrain
Roho yangu inaimba, nimefunguliwa kweli. Nimekaribia Yesu, ninaimba kwa furaha.
Couplet 2
Pepo za Neema yake zinavuma ndani yangu, na mawimbi ya Wokovu yananijaliza sasa.
Refrain
Roho yangu inaimba, nimefunguliwa kweli. Nimekaribia Yesu, ninaimba kwa furaha.
Couplet 3
Sasa Bwana Yesu Kristo amefanya kao kwangu. Nimepewa mfariji, Roho ya ahadi yake.
Refrain
Roho yangu inaimba, nimefunguliwa kweli. Nimekaribia Yesu, ninaimba kwa furaha.
Couplet 4
«Siku roho afikapo mtajua kwa hakika kwamba ninakaa kwenu», hivyo Yesu alisema.
Refrain
Roho yangu inaimba, nimefunguliwa kweli. Nimekaribia Yesu, ninaimba kwa furaha.
Couplet 5
Kweli, amefika kwetu, sasa yumo ndani yetu. Ujitoe kwake Mungu, aioshe roho yako!
Refrain
Roho yangu inaimba, nimefunguliwa kweli. Nimekaribia Yesu, ninaimba kwa furaha.
Couplet 6
Yesu atakapokuja katita utakatifu, nitafananishwa naye, nitamshukuru sana.
Refrain
Zitakuwa nyimbo nyingi tuta’poingia Mbingu, na milele tutaimba na kusifu Mungu wetu.