Indirimbo Zikundwa Open in the app

#36

Yesu ameniokoa, amenipa utulivu

Wokovu· S.L. Oberholzer, 1885

Couplet 1

Yesu ameniokoa, amenipa utulivu. Kwake ninaona raha, ninataka kumsifu.

Refrain

Haleluya, haleluya! Nimefika bandarini. Haleluya, haleluya! Jina lake ni mnara.

Couplet 2

Kwa furaha ninaimba wimbo mpya wa Wokovu. Nisichoke kamwe hapa kumwimbia Mkombozi.

Refrain

Haleluya, haleluya! Nimefika bandarini. Haleluya, haleluya! Jina lake ni mnara.

Couplet 3

Ni habari za Neema zakupasha pande zote. Mhubiri, enda mbio kufikia nchi zote!

Refrain

Haleluya, haleluya! Nimefika bandarini. Haleluya, haleluya! Jina lake ni mnara.

Couplet 4

Yesu, siku nita’kufa na maisha ni tayari, ’nichukue kwako juu penye raha ya milele!

Refrain

Haleluya, haleluya! Nimefika bandarini. Haleluya, haleluya! Jina lake ni mnara.