#34
Kwa pendo lake kubwa
Wokovu
Couplet 1
Kwa pendo lake kubwa alitafuta mimi, na alinichukua begani mazizini na nyimbo zao malaika zikajaza Mbingu pia.
Refrain
Alinitafuta, akaniokoa, akaniondoa matopeni, akanichukua mazizini.
Couplet 2
Mchunga Mwema Yesu aliniponya roho, na akaniambia: «Mtoto upendwaye». Sauti yake ya upendo ikaufariji moyo.
Refrain
Alinitafuta, akaniokoa, akaniondoa matopeni, akanichukua mazizini.
Couplet 3
Ninakumbuka jinsi alivyotoka Damu, na taji ya miiba, mateso ya mauti. Na penye Msalaba wake ninashukuru Bwana Yesu.
Refrain
Alinitafuta, akaniokoa, akaniondoa matopeni, akanichukua mazizini.
Couplet 4
Namfuata yeye katika nuru yake, waridi za ahadi zapamba njia yangu. Milele nitaendelea kusifu Yesu kwa furaha.
Refrain
Alinitafuta, akaniokoa, akaniondoa matopeni, akanichukua mazizini.
Couplet 5
Na saa zinapita, nangoja asubuhi utakaponiita, niende kwako juu. Nitasimama kwa amani Mbinguni mbele yako, Yesu.
Refrain
Alinitafuta, akaniokoa, akaniondoa matopeni, akanichukua mazizini.