Indirimbo Zikundwa Open in the app

#33

Huru kama ndege bustanini

Wokovu· Nils Frykman

Couplet 1

Huru kama ndege bustanini, sasa nafurahi kwa sababu Yesu ni rafiki yangu ’kubwa; nina amani siku zote.

Couplet 2

Aliniokoa na mashaka, alinipa tunu ya rehema. Mimi ni mtoto wa Babangu, na nuru inang’aa sana.

Couplet 3

Ninataka ku’shukuru Bwana, alitupa dhambi zangu mbali, na sitaziona tena kamwe, hazitanitawala tena.

Couplet 4

Jua likifichwa kwa mawingu, kiti cha rehema ni karibu, hayo ndipo shida ziishapo, na roho yangu yatulia.

Couplet 5

Radhi kama mwana kwa babake, kwa salama kama bandarini, Ninapumzika kwa Mwokozi, mbali na shida na huzuni.

Couplet 6

Yesu yu karibu siku zote, achukua mimi na mzigo. Napokea kwa mkono wake Neema na mateso pia.

Couplet 7

Nilimpa Yesu moyo wangu, ninapenda kumtumikia; neno lake linapendwa nami, na nira yake ni laini.

Couplet 8

Nafurahi sana kanisani kati ya watoto wa Babangu, Roho ya Neema ni karibu, kunanifurahisha sana.

Couplet 9

Mimi ni mdogo duniani, tena msafiri na mgeni. Kwetu ni Mbinguni huko juu; Babangu ananiongoza.

Couplet 10

Saa za mashaka zitakwisha, kuja kwake Yesu ni karibu. Nitaona raha kubwa sana katika nyumba ya Babangu.