Indirimbo Zikundwa Open in the app

#32

Hapo nilikuwa chini

Wokovu· James Rowe, 1912

Couplet 1

Hapo nilikuwa chini Katika dhambi nyingi, roho yangu iliona kufa na giza tele. Mungu alikisikia kilio changu huko, naye akanipandisha, kuniponya.

Refrain

:/: Nimeokoka, nimeokoka! Yesu Mwokozi wangu aliniokoa:/:

Couplet 2

Sasa Yesu amekuwa makimbilio yangu, na upendo wake ’kubwa uko moyoni mwangu. Ne’ma yake kubwa sana inajaliza roho, niwe mwaminifu kwake siku zote!

Refrain

:/: Nimeokoka, nimeokoka! Yesu Mwokozi wangu aliniokoa:/:

Couplet 3

Ewe, mwenye sikitiko, kuna matumaini: Yesu anakufahamu, atakusaidia. Atakupandisha toka tope la kuteleza, upokee ne’ma yake kwa Wokovu!

Refrain

:/: Nimeokoka, nimeokoka! Yesu Mwokozi wangu aliniokoa:/: