#31
Katika Safari yetu
Wokovu
Couplet 1
Katika Safari yetu kwenda huko juu tusilale usingizi, tuwe na bidii!
Refrain
Kaza mwendo tusifungwe, twende mbio tu! Yesu Kristo ni Mwokozi na Mfalme ’kuu!
Couplet 2
Bwana Yesu anatupa maji ya uzima, maji hai ya milele ya kuburudisha.
Refrain
Kaza mwendo tusifungwe, twende mbio tu! Yesu Kristo ni Mwokozi na Mfalme ’kuu!
Couplet 3
Njia na miiba mingi inatuzuia, hofu na hatari nyingi zina fadhaisha.
Refrain
Kaza mwendo tusifungwe, twende mbio tu! Yesu Kristo ni Mwokozi na Mfalme ’kuu!
Couplet 4
Mungu wetu atungoja huko kwake juu, Yesu ni Mwokozi wetu, tufuate Yeye!