#27
Una uhodari leo wa kumfuata Yesu
Wokovu
Couplet 1
Una uhodari leo wa kumfuata Yesu, hata ukichekwa sana na kuteswa duniani?
Couplet 2
Una uhodari leo kuwa mtu wake Mungu? Ukiona haya sana, kisha utaona nini?
Couplet 3
Mji unaonekana ukijengwa mlimani, hivyo na imani yetu inadhihirika sana.
Couplet 4
Ukipenda Yesu na kuliko vitu vyote, unataka kumkiri, mbele ya wenzako huku.
Couplet 5
Chuki au ’pendeleo kwako kitu bure tena, watafuta siku zote sifa zake Yesu Kristo.
Couplet 6
Ujihoji nafsi yako ukitaka kuokoka! Uliekataa Mungu, tubu dhambi zako leo!
Couplet 7
Umsihi masamaha, akuokoe ’kati Damu! Omba uhodari tena wa kumfuata Yesu!
Couplet 8
Uchague Yesu leo, uwe mfuasi wake! Ukitwaa Msalaba utaipokea taji!