Indirimbo Zikundwa Open in the app

#28

Ninataka kufuata wewe

Wokovu

Couplet 1

Ninataka kufuata wewe, Yesu, siku zote, ’kiwa katika furaha au shida na udhia. Unaponitangulia ninakuja nyuma mbio. Ninajua ni karibu Kuwasili huko kwako.

Couplet 2

Haifai niulize: Bwana, unakwenda wapi? Au kwa kusitasita kuishika njia yako. Kweli hapa kazi moja: Kufuata wewe mbio, kwenda njia ile moja wewe unionyeshayo.

Couplet 3

Walakini kama kitu kinataka kunifunga, au kuwa mgogoro katita safari yangu, ’kate kamba mara moja ifungayo roho yangu! Ninataka kuwa huru kukutumikia vema.

Couplet 4

Bwana Yesu, unilinde, uhifadhi nia yangu! Nikichoka kwa safari, nong’oneza kwa upendo: «Mwana, u mtoto wangu, uniandamie punde, utapumzika sana tena kwangu huko juu».