#22
Yesu Kristo Bwana wangu
Wokovu
Couplet 1
Yesu Kristo, Bwana wangu, una amri na uwezo za kuziondoa dhambi, na ’takasa roho yangu.
Refrain
’Nitolee masamaha, ’niokoe na jaribu, unilinde hata mwisho, unitwae kwako juu!
Couplet 2
Mbele nilikuwa mwovu, nilikukataa, Yesu, kwa hakika sikujua wewe na upendo wako.
Refrain
’Nitolee masamaha, ’niokoe na jaribu, unilinde hata mwisho, unitwae kwako juu!
Couplet 3
Bwana Yesu, usamehe dhambi nilizozifanya! Siitike majaribu, nguvu yako inilinde!
Refrain
’Nitolee masamaha, ’niokoe na jaribu, unilinde hata mwisho, unitwae kwako juu!
Couplet 4
Tangu sasa wewe, Yesu, u Mwokozi na rafiki, nimetengwa na shetani, niwe wako siku zote.