#21
Juu ya Mbingu zote
Wokovu
Couplet 1
Juu ya Mbingu zote, nyota na jua pia, hapo yafika kweli maombi ya mwenye dua. Roho ya mwanaDamu yamfikia Mungu, huko yabisha lango na kumtafuta Baba.
Couplet 2
Roho haitaona raha, amani huku; kuna bandari njema Mbinguni kwa Mungu Baba. Moyo utatulia, nuru itatokea tukifuata njia ya sala na maabudu.
Couplet 3
Hata mtoto ’dogo mwenye kuomba Mungu, hana la kuogopa; kuomba kwa faa sana. Tusisahau tena, pote twendako huku kwamba maombi yetu Yafika kwa Mungu Baba.