#20
Bwana Yesu, uniongoze
Wokovu
Couplet 1
Bwana Yesu, uniongoze baharini huku chini, juu ya mawimbi mengi, katika dhoruba kali! Bwana Yesu, uniongoze, nakutegemea wewe!
Couplet 2
Bwana Yesu, uniongoze, utulize moyo wangu! Neno moja toka kwako, mara shwari baharini. Bwana Yesu, uniongoze, nipe utulivu wako!
Couplet 3
Bwana Yesu, uniongoze, niyashinde majaribu! Mengi yakunidanganya, mengi ya kufunga macho! Bwana Yesu, uniongoze, niwe mshindaji kweli!
Couplet 4
Bwana Yesu, uniongoze, siku nita’vuka ng’ambo! Nikiona woga, giza, nipe nuru na amani! Bwana Yesu, uniongoze, uwe nami hata mwisho!