#16
Yo yote uonayo huku
Wokovu
Couplet 1
Yo yote uonayo huku katika mwendo wako, yafaa ku’mwambia Yesu, atakusaidia.
Refrain
Kwa kuwa kila aombaye Mwokozi Neema yake, ataokoka na hatia, na atasifu Yesu.
Couplet 2
Ukichukiwa na rafiki na ukijaribiwa, Mwokozi yu karibu sana, maombi asikia.
Refrain
Kwa kuwa kila aombaye Mwokozi Neema yake, ataokoka na hatia, na atasifu Yesu.
Couplet 3
Ukiwa mwana mpotevu, na mbali na babako, amani una’kosa sasa, urudi kwake Yesu!
Refrain
Kwa kuwa kila aombaye Mwokozi Neema yake, ataokoka na hatia, na atasifu Yesu.
Couplet 4
Ukiwa na makosa mengi, na roho yako ngumu, Neema yake yakutosha, utubu dhambi zako!
Refrain
Kwa kuwa kila aombaye Mwokozi Neema yake, ataokoka na hatia, na atasifu Yesu.
Couplet 5
Ikiwa nguvu mara nyingi kuomba kwa bidii, uombe Baba, kama mwana, akusikia kweli!